Safari bado ni ndefu kwa nchi maskini kujikwamua na umaskini

Kusikiliza /

S.-M.-Krishna

Nchi zinazoendelea bado zina changamoto kubwa katika kutokomeza umaskini na kuwa na maendeleo endelevu. Kauli hiyo imo kwenye hotuba ya Waziri wa Mambo ya Nje wa India, S. M Krishna aliyoisoma Jumatatu kwenye mkutano wa 67 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani.

Ametolea mfano nchi za Afrika Kaskazini na Magharibi mwa bara la Asia ambazo amesema zinashuhudia mgogoro wa aina yake wa kijamii na kisiasa kwa kuwa bado zinahangaika kujikwamua na madhara ya mdororo wa kiuchumi huku masuala ya chakula, afya, elimu na nishati yakibakia changamoto kubwa.

Waziri huyo wa Mambo ya Nje wa India pia amezungumzia shughuli za Umoja wa Mataifa za kulinda amani ambapo amesema nchi yake imeshiriki katika operesheni 43 tangu miaka ya 1950 na kwamba changamoto sasa ni kuhakikisha operesheni hizo zinapatiwa rasilimali za kutosha.

Krishna pia ameungana na mataifa mengine kutaka marekebisho ya muundo wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambapo amesema kinachotakiwa ni kuongeza idadi ya wajumbe wa kudumu na wale wasio wa kudumu.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2013
T N T K J M P
« apr    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031