Rushwa kwenye mifumo ya mahakama ni kitisho kwa haki za binadamu asema Mtaalamu wa UM

Kusikiliza /

Gabriela Knaul

Kushamiri kwa vitendo vya rushwa kwenye mifumo ya kimahakama kunazua kitisho ambacho kinazorotesha haki za binadamu, ameonya mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa.

Mtaalamu huyo Gabriela Knaul, amezitolea mwito serikali duniani kote kuanisha na kutekeleza sera zitakazoboresha utawala bora akisema kuwa hatua hiyo itasaidia kubinya mianya ya rushwa.

Amesema wakati huu kunashuhudiwa ongezeko kubwa la vitendo vya rushwa kwenye mifumo ya utoaji haki na maamuzi kama mahakama jambo ambalo siyo tu linakwaza ustawi wa kijamii lakini pia linakwamisha juhudi za kuboresha haki za binadamu.

Bi. Knaul amesema kuwepo vitendo vya rushwa katika mifumo ya kimahakama kunawakwaza na kuwabinya waathirika wa matukio ya uvunjifu wa haki za binadamu ambao wanakosa msaada wala mwongozo katika jamii zao.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031