Ripoti yadhihirisha ukiukwaji wa haki za binadamu Nepal: UM

Kusikiliza /

Navi Pillay

Tume ya haki za bindamu ya Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu, leo imetoa ripoti ya aina yake inayoelezea bayana vitendo vya ukiukwaji wa sheria ya kimataifa wakati wa kipindi miaka kumi ya mgogoro nchini Nepal kuanzia mwaka 1996 hadi 2006.

Katika utangulizi wake kwenye ripoti hiyo ya kurasa 233, Mkuu wa tume hiyo Navi Pillay amesema nyaraka takribani Elfu Thelathini katika ripoti hiyo zitasaidia taasisi nchini Nepal ikiwemo zile za kiraia kuanzisha mchakato wa kubaini ukweli, haki na maridhiano kwa vitendo hivyo vya kihalifu vilivyofanyika kwenye kipindi hicho. Taarifa zaidi na George Njogopa.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031