Navi Pillay alaani hatua ya upitishwaji wa sheria kandamizi Ukraine

Kusikiliza /

Navi Pillay

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu Navi Pillay amelaani na kushurtumu uamuzi iliochukuliwa na bunge la Ukraine ya kuweka kusudio la kupitisga sheria ambayo inapiga marafuku vitendo vya ushoga.

Mswaada huo wenye nambari 8711 kama utapitishwa na kuwa sheria utawatia hatiana wahusika wa vitendo vya ushoga vinavyofanywa hadharani kutozwa faini ama kifungo cha hadi miaka mitano.

Sheria hiyo ambayo imelenga kubana vitendo vyote vya ushoga inatajwa kuwa ni ya kibaguzi na inakwenda kinyume na maaazimio ya kimataifa yanayohimiza uhuru wa maoni na kupokea habari.

Wale wote watakabainika kutumia vyombo vya habari kupenyeza tabia zenye mafungamano ya ushoga wataandamwa na sheria hiyo mpya ambayo inakusudiwa kufanyiwa marekebisho hivi karibuni.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031