Nafasi ya posta bado iko pale pale licha ya maendeleo ya teknolojia: Profesa Tibaijuka

Kusikiliza /

Professa Ann Tibaijuka

Balozi maalum wa anwani za makazi wa Umoja wa Mashirika ya posta duniani, UPU, Profesa Anna Tibaijuka, amesema kongamano la 25 la umoja huo limekubaliana kuwa huduma za posta zitaendelea kuwa na umuhimu mkubwa duniani licha ya maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano.

Profesa Tibaijuka ameiambia Radio ya Umoja wa Mataifa kuwa katika kongamano hilo, utashi wa kisiasa miongoni mwa nchi 192 wanachama wa Umoja huo ulikuwa dhahiri kwa kuzingatia kuwa kilichobadilika ni mfumo wa huduma za posta na si kuachana na huduma hiyo na tayari nchi zimewekeza katika mradi wa anwani za makazi.

(SAUTI YA ANN TIBAIJUKA)

Mkutano huo pia ulishuhudia kuchaguliwa kwa Bishar Hussein kutoka Kenya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa UPU kuanzia mwakani ambapo anachukua nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa sasa Edouard Dayan anayestaafu baada ya kuhudumu kwa kipindi cha miaka minane.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031