Muziki utumike kueneza ujumbe wa amani duniani kote: Jeremić

Kusikiliza /

Stevie Wonder na Katibu Mkuu wa UM

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Vuk Jeremic amesema amani ya kweli haitokani na kutokuwepo kwa vita pekee, bali amani ya kweli ni matokeo ya maridhiano yaletwayo na kuombana msamaha. Bwana Jeremic amesema hayo Jumatano usiku kwenye Makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York wakati wa tamasha maalum la muziki la kuadhimisha siku ya Umoja huo ambapo mjumbe wa amani wa Umoja wa Mataifa Stevie Wonder na rafiki zake wametumbuiza.

Ametolea mfano nyimbo za Stevie Wonder ambazo amesema kila wakati zimekuwa zikigusia masuala ya amani na kusema kuwa ni matumaini yake katika siku ya Umoja wa Mataifa, Muziki ambao ni lugha inayounganisha watu wote duniani, utatumika kueneza amani.

"Wito wa amani na maelewano ni ujumbe wa mara kwa mara wa muziki wa Steve Wonder. Kila mara ujumbe tunaosikia ni ule kwamba mtu anapotafuta amani anapaswa kuanza na yeye mwenyewe. Kujenga dunia ya haki, wewe mwenyewe unapaswa kutoa haki. Kujenga jamii yenye uvumilivu, wewe mwenyewe unapaswa kuwa mvumiliv. Mtu hawezi kumlazimisha mtu ajitoe kwa ajili ya amani iwapo yeye mwenyewe hayuko tayari kufanya hivyo. Ndio maana amani haiwezi kuwa matokeo ya hofu au kulazimishwa kufanya kitu."

Wakati wa tamasha hilo Stevie Wonder ametumbuiza nyimbo zake mashuhuri ikiwa ni sehemu ya kusherehekea kazi za Umoja wa Mataifa duniani kama vile kutoa misaada ya kibinadamu, usawa wa kijinsia, haki za binadamu, ulinzi wa amani na huduma kwa wakimbizi.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031