Muungano wa Ulaya watoa Euro millioni 11 kuwasaidia wakimbizi wa Palestina

Kusikiliza /

wakimbizi wa Palestine

Shirika la Mungano wa Ulaya linalohusika na msaada kwa kibinadam (ECHO) leo limetangaza msaada wake wa millioni kumi na moja kwa Shirika la Umoja wa Mataifa wa linalowasaidia wakimbizi wa Palestina (UNRWA). Msaada huo utasaida shirika la UNRWA kufanya katika shughuli zake nchini Syria, Lebanon naPalestina.

Mkuu wa UNRWA, Bwana Filippo Grandi, amesema Mungano wa Ulaya umekuwa msaidizi mwema daima kwa kutoa msaada wa waPalestina kwa zaidi ya miaka kumi. Msaada huu umekujaa wakati muhimu, hasa wakati huu ambapo kazi ya Shirika la UNRWA inaendelea kuwa na walengwa zaidi.

Fedha hizi zinafuatia msaada wa zamani, ambapo Mungano wa Ulaya ulitoa msaada wa Euro millioni 8.7 kwa ajili ya usaidizi wa kibinadamu kwa watu wa Palestina, na Euro millioni 1.2 kwa kazi ya shirika hilo huko Lebanon. Euro millioni sita itatumika kwa matumizi ya chakula huko Gaza, ambapo watu 735,000 hawana chakula, hasa watoto, kwa kusambaza chakula shuleni.

Mgogoro unaoendelea kuenea nchini Syria umeathiri wakimbizi 225,000 wa Palestina.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031