Mtaalamu wa Canada ateuliwa kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amemteua Bwana David Malone raia wa Canada kuwa mwangalizi wa chuo kikuu cha Umoja wa Mataifa, kufuatia majadiliano aliyofanya na Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Irina Bokova.

Bwana Malone anatazamiwa kuwa mkuu wa sita wa chuo hicho ambacho kinawaleta pamoja wasomi kutoka sehemu mbalimbali dunia wanaotumika kama chachu ya mawazo kwa Umoja wa Mataifa.

Anatazamiwa kuchukua wadhifa huo kuanzia March 1, mwaka ujao 2013, akichukua nafasi itakayoachwa na mtangulizi wake Konrad Osterwalder aliyedumu kwenye wadhifa huo tangu mwaka 2007.

Kabla ya uteuzi huo Bwana Malone amekuwa akifanya kazi katika kituo cha kimataifa kinachojihusisha na utafititi wa kimaendeleo akiwa kama rais wa taasisi hiyo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031