Mshindi wa tuzo ya sanaa kwa ajili ya amani atunukiwa

Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, leo amemkabidhi tuzo mshindi wa shindano la sanaa kwa ajili ya amani, Bi Haruka Shoji, katika hafla ilofanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York. Shindano hilo la sanaa kwa ajili ya amani liliandaliwa na afisi ya masuala ya kuondoa silaha ya Umoja wa Mataifa na wakfu wa kuungana kwa ajili ya amani.

Wagombea wa shindano hilo walihitajika kuchora picha inayoonyesha ulimwengu usio na silaha za nyuklia, mabomu , vita au hofu. Wagombe walihitajika kutizama filamu fupi kwenye tovuti, na kubuni mchoro kutokana na walichokiona kwenye filamu hiyo na maudhui ya shindano.

Haruka Shoji ambaye ni mshindi atapokea zawadi ya fedha na cheti kutoka kwa Umoja wa Mataifa, na mchoro wake utachapishwa kwenye kalenda ya Umoja wa Mataifa.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031