Msaada zaidi wahitajika baada ya mafuriko nchini Pakistani:IOM

Kusikiliza /

mafuriko nchini Pakistan

Licha ya kwamba vifaa vya msaada vimeanza kuwasili kwenye maeneo yaliyokumbwa na mafuriko nchini PAKISTANI, Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limeonya kuwa msaada zaidi unahitajika ili kukidhi mahitaji yaliyobainishwa na ofisi ya majanga nchini humo.

Maria Moita kutoka IOM ambayo inaratibu usambazaji wa misaada kwa waathirika wa mafuriko, amesema shughuli za usaidizi zinakwamishwa na uhaba wa fedha na kwamba vifaa vya msaada vinamalizika hivyo fedha zaidi zahitajika kupata vifaa vya kuwapatia waliokumbwa na mafuriko.

Tayari IOM imesambaza mahema Elfu Moja kwenye wilaya za Rajanpur na Dera Ghazi huko Punjab na vifaa vingine ikiwemo taa, mablanketi na vifaa vya jikoni hivi sasa vinapelekwa huko Sindh na Balochistan.

Takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya watu Milioni Mbili na Nusu wameathiriwa na mafuriko nchini Pakistani yaliyosababisha vifo vya watu 422 na nyumba 270,000 kusombwa na maji wakati huu ambapo ni chini ya asilimia 19 tu ya mahitaji ya msaada yaliyobainishwa na Pakistan ndiyo yamepatikana.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031