Mkuu wa IMF ataka ushirikiano zaidi na marekebisho katika mfumo wa fedha

Kusikiliza /

Christine Lagarde

Mkuu wa shirika la fedha duniani, IMF, Christine Lagarde, amesema mbali na kujikwamua kutoka kwenye mdororo wa uchumi uliopo sasa, siku za baadaye za uchumi wa kimataifa zitategemea ushirikiano zaidi na kurekebisha mfumo wa fedha. Bi Lagarde amesema hayo katika mikutano ya IMF na Benki ya dunia inayoendelea mjini Tokyo, Japan.

Amesema kuwa ulimwengu una uhusiano wa kutegemeana, na hivyo ni lazima ufanye kazi kwa kushirikiana, huku akitaja umuhimu wa taasisi za kimataifa kama IMF, ambazo, amesema zinawakilisha ushirikiano kama huo kwa njia ya kipekee.

Kwa sababu hiyo, amesema IMF ni lazima ionekane kama taasisi inayouawakilisha ulimwengu, inayoaminika, inayosimama bega kwa bega na wanachama wake, na ambayo ina sura ya kumilikiwa kimataifa. Ameongeza kuwa ili mfumo bora zaidi wa fedha ni muhimu katika uchumi wa kimataifa siku hizi, na hivyo ni inahitajika kuondokana na mfumo ulioutosa ulimwengu katika mdororo uliomo sasa, na kuufanyia marekebisho yanayofaa.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031