Mkutano wafanyika Nairobi kuelewa mahakama za kijeshi

Kusikiliza /

majaji, Mogadishu

Majaji kutoka mahakama za kijeshi mjini Mogadishu wamekutana na wawakilishi kutoka jamii ya kimataifa mjini Nairobi ili kufanya mazungumzo kwa ajili ya kuelewa vyema zaidi hali katika mfumo wa kijeshi.

Mkutano huo ambao umeandaliwa na afisi ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Somalia, UNPOS, umetambua ni vipi usaidizi wa Umoja wa Mataifa na wafadhili wengine unaweza kutumika kuimarisha kuheshimu haki za binadamu katika mfumo wa mahakama za kijeshi.

Mahakama ya kijeshi imekuwa na jukumu muhimu la kuhakikisha uwajibikaji kisheria wakati wa migogoro ya silaha nchini Somalia, kwani mfumo wa haki wa kiraia haujakuwa na uwezo wa kukabiliana na uhalifu wa kupangwa unaotekelezwa na makundi yenye silaha. Majaji wanaokabiliana na kesi kama hizo hukumbwa na hatari na vitisho kila wakati. Joshua Mmali na taarifa kamili.

(SAUTI YA JOSHUA MMALI)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031