Mkutano wa FAO kuhusu usalama wa chakula waanza mjini Roma

Kusikiliza /

Nwanze Kanayo

Kamati inayohusika na usalama wa chakula ya Shirika la Kilimo na Chakula, FAO, imeanza mikutano yake ya wiki moja hii leo katika makao makuu ya FAO mjini Roma, Italia, siku moja kabla ya Siku ya Chakula Duniani, ambayo huadhimishwa kila tarehe 16 Oktoba. Kamati hiyo ndilo jukwaa la jumla serikali za kimataifa, mashirika ya umma, wataalam na wadau wengine wanaoshirikiana kuhakikisha kuwepo kwa usalama wa chakula na lishe kwa wote.

Majadiliano kwenye mikutano ya kamati hiyo ambayo itaendelea hadi Jumamosi Oktpba 20, yataangazia ulinzi wa kijamii kwa ajili ya usalama wa chakula, pamoja na usalama wa chakula katika mazingira ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Wajumbe watatu wa Kamati ya Maendeleo pia wanahudhuria mikutano hiyo, na watawasilisha mapendekezo yaliyoidhinishwa katika maazimio ya kamati hiyo kuhusu hali katika Pembe ya Afrika na usalama wa chakula, ambayo yanatoa wito kwa Jumuiya ya Nchi za Ulaya, EU, kuzingatia kuwekeza zaidi katika kilimo na maendeleo katika kilimo.

Akizungumza kwenye mkutano huo, rais wa hazina ya kimataifa ya maendeleo ya kilimo, IFAD, Kanayo Nwanze, amesema wakulima wadogo wanahitaji vifaa vya kutumia ili kuongeza uzalishaji wao.

(SAUTI YA KANAYO NWANZE)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031