Mjumbe wa mzozo wa Syria ahitimisha ziara Uturuki

Kusikiliza /

Lakhdar Brahimi

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya nchi za kiarabu katika mzozo wa Syria, Lakhdar Brahimi, amehitimisha ziara Uturuki kwa kuwa na majadiliano na rais Abdullah Gul na waziri wa Mambo ya Nje Ahmet Davutoglu.

Viongozi wamekubaliana haja ya kukomesha uhasama wa pande mbili ambazo hivi karibuni zilifurumishiana makombora ikiwa jitihada za kila sehemu kujihami na upande mwingine.

Tangu kuzuka kwa mkwamo huo nchini Syria kiasi cha watu 20,000 wamepoteza maisha na mamia wengine wakikimbilia uhamishoni.

Hali ya kibinadamu inazidi kuzorota na ripoti zinasema kuwa zaidi ya watu milioni 2 wako kwenye mkwamo wa kibinadamu.

Akiwa nchini Uturuki. Bwana Brahimi alikutana na kufanya mazungumzo na mwenyekiti wa baraza la taifa la upinzani la Syria Abdel Bassett Sida,pamoja na wajumbe wengine wa baraza hilo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031