Mgogoro wa Syria ni kengele kwa UM kutekeleza shabahaya mageuzi:Mawaziri wa Ulaya

Kusikiliza /

Aurelia Frick

Katika wakati hali ikizidi kuchacha nchini Syria kwa mamia ya watu kuendelea kupoteza maisha wengine wakilazimika kuimbilia uhamishoni, hiyo ni alama inayoonyesha umuhimu wa kuwepo kwa mageuzi ndani ya Umoja wa Mataifa ili chombo hicho kiwe na uwezo wa kudhibiti hali yoyote korofi kutojitokeza.

Hayo ni kwa mujibu wa wanadiplomasia wa Ulaya ambao wamekimbia kikao cha baraza kuu la Umoja wa Mataifa kuwa chombo hicho cha kimataifa kinapaswa kufanyiwa mageuzi.

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Iceland Össur Skarphéðinsson ameliambia baraza hilo kuwa yale yanayoendelea kushuhudia nchini Syria ni kengele kwa Umoja wa Mataifa ambao unapaswa kuamka na kujikagua kama kweli inakwenda sambamba na matarajio yake.

Kiasi cha watu 18,000 wamepoteza maisha nchini Syria na wengine maelfu kadhaa wakikimbilia uhamishoni kutokana na mapigano makali yanayoendelea kushuhudia baina vikosi vya serikali na makundi ya waasi.

Wito kama huo umetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Montenegro Nebojša Kaluderovic ambaye ameitupia lawama Israel kwa kuendesha mashambulizi ya mara kwa mara katika ukingo wa Gaza. Naye ametaka Umoja wa Mataifa kukaribisha mageuzi.

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031