Maldives yataka pande husika zitulie katika mauaji ya mbunge:IPU

Kusikiliza /

bendera za wanachama wa IPU

Umoja wa mabunge duniani, IPU umeshutumu mauaji ya leo ya mbunge wa chama cha Progressive Party of Maldives, PPM nchini Maldives Afrasheem Ali.

Mauaji hayo ya punde zaidi na ya kwanza kwa mbunge yameelezwa kuwa ni ya kutisha katika mfululuzo wa ghasia zilizokumba visiwa hivyo tangu kuanza kwa mzozo wa kisiasa mapema mwaka huu huu.

IPU imesema imetaka kumalizwa kwa ghasia hizo na pande zote husika kutulia wakati huu ambapo umoja huo unapata wasiwasi kutokana na wabunge zaidi kupokea ujumbe wa vitisho vya kuuawa kupitia vyombo vya habari vya kijamii kama vile Twitter.

Kutokana na ghasia, manyanyaso na vitisho vya kisiasa wanavyokumbana navyo, wabunge kadhaa wa Maldives wamejisajili katika Kamati ya Haki za Binadamu ya IPU.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031