Mataifa madogo yanaweza kuchangia amani na usalama wa kimataifa:Ban
Kusikiliza /Licha ya udogo wao, mataifa madogo yanaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa amani na usalama duniani, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon.
Bwana Ban amesema hayo kwenye kongamano kuhusu mataifa madogo, ambalo limeandaliwa na Jumuiya ya Mataifa Madogo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.
Bwana Ban amesema, kwa kipindi cha miaka 20 ilopita, jumuiya hiyo ya mataifa madogo imechangia kwa kiasi kikubwa katika mazungumzo na sera za kimataifa.
(SAUTI YA BAN KI-MOON)
Katibu Mkuu amesema pia mataifa hayo madogo yanayoendelea hukabiliwa na changamoto nyingi, lakini bado yametoa mchango wa upatanishi na kumlikia masuala ambayo yanayaathiri mataifa makubwa na madogo. Amesema Umoja wa Mataifa utaendelea kuyazingatia matakwa ya mataifa haya kwa njia maalum.
