Mataifa yaliyo Pacific yajadili uchumi na nishati

Kusikiliza /

Mkutano wa siku mbili wa mataifa Kumi na Nne ambayo ni visiwa katika bahari ya Pacific umemalizika huko Fiji kwa kutambua umuhimu wa nchi hizo kuunganisha sera zao za uchumi mkuu na zile za usalama wa nishati ili kuwa na maendeleo endelevu na kuepuka uchumi wao kutikiswa na athari za nje.

Maafisa zaidi ya 50 wakiwemo wataalamu wa fedha, mipango na nishati pamoja na washirika wa maendeleo walishiriki mkutano huo wa kisera ulioandaliwa na Tume ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya kiuchumi na kijamii kwa mataifa ya Asia na Pacific, ESCAP ambapo walitambua pia azma ya viongozi wa dunia katika mkutano wa Rio+20 wa kuweka mizania ya misingi ya uchumi, jamii na mazingira kwa maendeleo endelevu.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031