Mashambulizi ya walowezi wa Israeli dhidi ya wapalestina hayakubaliki: UM

Kusikiliza /

Robert Serry

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa katika mpango wa amani wa Mashariki ya Kati, Robert Serry ameeleza kushtushwa kwake na ripoti kuwa walowezi wa kiisraeli wamekuwa wakishambulia mara kwa mara wakulima wa kipalestina katika Ukingo wa Magharibi wa mto Jordan na kuharibu miti ya mizeituni wakati huu wa msimu wa mavuno.

Serry amesema kitendo hicho hakifai na ameitaka serikali ya Israel kuwafikisha mbele ya sheria wahusika wote huku ikizingatia ahadi yake ya kulinda wapalestina pamoja na mali zao. Assumpta Massoi na taarifa zaidi.

(SAUTI YA ASSUMPTA MASSOI)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031