Maneno ya Roosevelt bado ni muhimu hata sasa: Ban

Kusikiliza /

Miaka 60 tangu Rais wa zamani wa Marekani, hayati Franklin Delano Roosevelt ataje aina nne za uhuru, mpaka sasa maneno yake hayo yamebakia mwongozo kwa watu duniani kote.

Hiyo ni kauli ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon aliyoitoa leo jijini New York, Marekani wakati wa hafla ya kuipatia bustani moja karibu na makao makuu ya Umoja wa Mataifa jina la kiongozi huyo aliyekuwa mstari wa mbele katika kuanzishwa kwa Umoja huo.

Uhuru aliotaja hayati Roosevelt ni ule wa kujieleza, kuabudu na kuishi bila woga na uhuru wa kuishi maisha yenye staha.

“Rais Roosevelt aliongozwa na dira ya kimataifa. Alielewa kuwa ndoto za binadamu hazibanwi na hati ya kusafiria ya mtu huyo. Alielewa kuwa matamanio ya mtu hayawezi kudhibitiwa na mipaka ya kitaifa. Na pia aliamini kwa dhati kuwa viongozi popote walipo wanapaswa kusaidia watu watimize ndoto zao. Hakuna kinachozungumza zaidi ya maneno hayo kuhusu haki na uhuru.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031