Mamia ya raia wa Colombia kunufaika na mpango wa kuondokana na umaskini

Kevin Cleaver

Zaidi ya familia 50,000 nchini Colombia zinatazamiwa kunufaika na mpango mpya unaoendwa na Umoja wa Mataifa wenye shabaha ya kukabiliana na hali ya umaskini katika maeneo ya vijijni.

Chini ya mpango huo familia hizo zinatazamiwa kufikiwa na misaada ya kifedha ili hatimaye ziendesha miradi ya ujasiliamali ambao unaelezwa unasaidia kuwavusha kutoka daraja la chini hadi lile la kujimudu kimaisha.

Zaidi ya watu milioni saba nchini humo wanatajwa kuishi chini ya kiwango cha umaskini wakati kiasi cha watu milioni mbili ni maskini wa kutupwa.

Takwimu zilizotolewa na shirika la kimataifa IFAD, zinaonyesha kuwa karibu asilimia 13 ya watu wote nchini humo hawana vyanzo mbadala ya kujipatia kipato kwa ajili ya mahitaji yao ya kila siku kama chakula.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031