Malaria bado ni tishio barani Afrika, msaada zaidi wahitajika: Tanzania

Kusikiliza /

ugonjwa wa malaria barani Afrika

Ugonjwa wa Malaria umeelezwa kuwa bado ni tishio barani Afrika kutokana na vikwazo mbali mbali licha ya utashi wa kisiasa wa kutokomeza ugonjwa huo hivyo msaada zaidi wa wataalamu na vifaa tiba unahitajika.

Kauli hiyo ni ya Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Mahadhi Juma Maalim aliyotoa alipozungumza na Radio ya Umoja wa Mataifa baada ya kuwasilisha ripoti ya Tanzania juu ya kupambana na Malaria mbele ya kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, kilichoketi siku ya kwanza ya juma la Afrika na mada kuu ikiwa muongo mmoja wa kupambana na Malaria.

Mahadhi amesema serikali kama Tanzania inajitahidi kwa uwezo wake mathalani baadhi ya maeneo kiwango cha kuenea malaria kinakaribia Sifuri lakini kwenye maeneo mengine bado hali si nzuri hivyo ameliomba baraza la Kuu la Umoja wa Mataifa kutoa msaada zaidi.

"Mfumo wetu wa uchumi, mfumo wetu wa kimaisha peke yake nao unaleta changamoto hiyo. Lakini jingine ni kwamba hata wakati serikali inapochukua jitihada mfano ya ya kusambaza hivyo vyandarua, tumekuta kesi nyingi tu ambapo badala ya kuvitumia vyandarua hivyo kwa malengo lililokusudiwa wengine wamekuwa wakviitumai kinyume ya malengo, kwa hiyo uelewa wa watu bado, kuna sehemu mtu anawezekana anaumwa malaria,mtoto anaumwa malaria, badala ya kumuwahisha hospitali bado anafikiriwa labdal ni mazingira au ni hali kwamba kuna uchawi au kwamba labda maradhi mengine yanaweza kutibika kwa dawa zingine ambazo si sahihi, hayo yote yamekuwa ni vikwanzo ni changamoto katika kupambana na malaria."

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031