Makazi mapya kusaidia wahamiaji wavulana na wasichana huko Afrika Kusini: IOM

Kusikiliza /

wahamiaji Afrika Kusini

Katika hatua nyingine ofisi ya IOM nchini Afrika Kusini Jumatatu itakabidhi makazi mapya na yaliyokarabatiwa kwa ajili ya wahamiaji wavulana wanaosafiri wenyewe pamoja na wasichana walio katika mazingira hatarishi ikiwa ni sehemu ya mradi wa kuweka amani na mtangamano baina ya jamii zenye asili tofauti.

IOM imesema makazi hayo huko Musina mpakani kwa Afrika Kusini na Zimbabwe, yatahudumia wavulana 200 na wasichana 80 na ukarabati wake umetokana na mradi uliofadhiliwa na Tume ya Ulaya, shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa na serikali ya Afrika Kusini.

Tangu mwaka 2008, makazi hayo ya muda ya Musina yameshuhudia kuwasili kwa wahamiaji watoto wanaosafiri peke yao pamoja na wahamiaji wengine walio katika mazingira hatarishi ikiwemo wanawake na wasichana waliokumbwa na manyanyaso ya kijinsia.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031