Majeshi ya AU nchini Somalia yapatiwe msaada: Balozi Mahiga

Kusikiliza /

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa hii leo limeombwa kukubali ombi la Umoja wa Afrika, AU, la kuimarisha ulinzi wake eneo la baharini huko Somalia.

Ombi hilo limewasilishwa na Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Dkt. Augustine Mahiga alipohutubia kwa njia ya video baraza hilo kutoka mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

Amesema kikosi maalum cha Umoja wa Afrika nchini Somalia, AMISOM kimezidiwa uwezo katika utekelezaji wa majukumu yake licha ya askari wa ziada na vifaa kupelekwa nchini Somalia.

Dkt. Mahiga amesema kwa kuwa vikosi vya AU na vile vya Somalia vinadhibiti eneo kubwa, bila shaka vinapaswa kuwa na vifaa bora zaidi kukabiliana na wanamgambo wa Al-Shabaab.

Ni muhimu pia AMISOM ikasaidiwa ili idhibiti vyema zaidi eneo la majini lililo karibu na pwani ya Mogadishu, Merca, Barawa na Kismayo na iweze kulinda askari wake, mifumo yake ya kusambaza vifaa na kuharibu mifumo ya usambazaji ya Al-Shabaab na hatimaye kushikilia bandari kwa matumizi ya kibiashara na kuzuia biashara ya makaa."

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2017
T N T K J M P
« dis    
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031