Mafuriko nchini Chad yalazimu wakimbizi kuhamishwa: UNHCR

Kusikiliza /

mafuriko nchini Chad

Huko Kusini mwa C, mafuriko yamelazimu Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, pamoja na washirika wake kuwahamishia maeneo yaliyo kwenye mwinuko wakimbizi wapatao Elfu Kumi na Saba kutoka kambi za Yaroungou na Moula.

Mathalani katika kambi ya Yaroungou mafuriko yameharibu asilimia 85 ya mahindi na mpunga na hifadhi ya chakula na mbegu zimesombwa na maji wakati huu ambapo karibu nchi nzima ya Chad imeathiriwa na mafuriko hayo.

Wakimbizi hao kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati walilazimika kukimbilia uhamishoni mwaka 2003 na 2008 kutokana na mgogoro wa kivita na mizozo ya kisiasa nchini mwao.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031