Madagascar yakabiliwa na uhaba wa chakula: WFP

Kusikiliza /

uhaba wa chakula, Madagascar

Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP limesema idadi ya watu wanaokabiliwa na uhaba wa chakula nchini Madagascar imeongezeka na kufikia asilimia 33 ya wananchi wote nchini humo..

Msemaji wa WFP Elizabeth Byrs amesema hayo mjini Geneva, Uswisi leo alipozungumza na waandishi wa habari ambapo amesema malengo ya shirika hilo ni kuwapatia chakula watu Milioni Moja ifikapo mwakani.

"WFP nchini Madagascar imepanga kufikia watu Milioni Moja mwaka 2013. Hatujaongeza idadi ya watu tutakaowapatia msaada wa chakula kwa sababu mwaka 2012 tulisaidia pia watu Milioni Moja. Lakini bado tunahitaji misaada zaidi kwa sababu mipango yetu inahitajika sana hususan kuna watoto zaid iya Milioni Moja wenye umri wa kwenda shule lakini kwa sasa hawako shule kutokana na tatizo la sasa."

Ametaja sababu za uhaba wa chakula nchini Madagascar kuwa ni migogoro ya kisiasa, kuporomoka kwa uchumi, umaskini wa kupindukia, majanga ya kiasili pamoja na kukosekana kwa huduma za msingi za kijamii.

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031