Katika kuadhimisha siku ya miji duniani, UM wasema kuboresha miji kunaboresha maisha

Kusikiliza /

familia nchini Kenya

Nusu ya idadi ya watu kote duniani wanakaa mijini, na kadri idadi hii inavyoendelea kuongezeka, ndivyo juhudi zaidi zinafaa kufanywa ili kupunguza umaskini mijini na kuweka maendeleo endelevu. Huo ndio ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon kwenye siku ya makazi ya mijini duniani, ambayo huadhimishwa kila Jumatatu ya kwanza ya mwezi wa Oktoba.

Siku hii iliwekwa na Umoja wa Mataifa ili ulimwengu utafakari kuhusu hali ya makazi mijini, na haki ya kila mmoja kuwa na makaiz yanayofaa sasa na siku zijazo. Kauli mbiu ya mwaka huu ni "kubadili miji ni kuweka nafasi zaidi za ukuaji". Umoja wa Mataifa unautumia ujumbe huu kama chagizo la kuipanga miji vyema zaidi kwani miji isiyopangwa vizuri inachangia ukuaji wa kiholela.

Naye mtaalam wa Umoja wa Mataifa kuhusu makazi yanayofaa Raquel Rolnik, amesema mfumo wa kuendeleza mikopo kama njia ya watu kuweza kumiliki nyumba haufanyi kazi kama inavyodhaniwa na wengi. Katika mahojiano na Radio ya Umoja wa Mataifa, Bi Rolnik amesema kuweka mbele pesa katika umiliki wa nyumba kunawafaa wachache tu.

(SAUTI YA ..

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031