Kufuatia mafuriko ya Benin, Jumuiya ya kimataifa yasaka njia mpya kuwasaidia waathirika

Kusikiliza /

Mafuriko Benin

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa na ule wa Jumuiya ya nchi za kiislamu OIC ambao ulikuwa nchini Benin kutathmini hali mbaya iliyosababishwa na mafuriko ya hivi karibuni umejadilia haja ya kutumwa misaada ya dharura kuwanusuru mamia ya watu ambao maisha yao yako taabani.

 Ujumbe huo ulikuwa nchini humo kwa siku tatu na kutathmini hali jumla ya mambo tangu nchi hiyo ikumbwe na mafuriko makubwa umependekezwa kuchukuliwa kwa njia mpya ya kuwasaidia wakazi wa eneo hilo.

 Mratibu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na misaada ya kiutu OCHA, Bwana Paschal Karorero amesema kuwa ziara ya ujumbe huo imekuja wakati muafaka wakati ambapo kunashuhudiwa mahitajio makubwa ya misaada ya dharura.

 Afisa huyo amesema kuwa pamoja na mkwamo huo lakini jambo la msingi linalopaswa kuzingatiwa sasa ni kuandaliwa kwa njia mpya itayotoa matumaini mapya kwa mamia ya wananchi amabo makazi yao yameharibiwa na mafuriko hayo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031