Kongamano la utalii barani Afrika laanza nchini Tanzania

Kusikiliza /

utalii nchini Tanzania

Wataalamu wa masuala ya utalii barani afrika leo wanaanza kongamano la siku tano nchini Tanzania ambalo pamoja na mambo mengine linatazamiwa kujadilia usimamizi wa utalii endelevu katika hifadhi za taifa.

Kongamano hilo ambalo limeandaliwa kwa ushirikiano kati ya serikali ya Tanzania na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na utalii linahudhuriwa na wajumbe zaidi ya 400 kutoka barani afrika na nje ya bara hilo.

Kutoka DSM, Mwandishi wetu George Njogopa ameaandaa taarifa ifuatayo.

Kongamano hilo linafanyika katika wakati ambapo hali ya utali kwa nchi za afrika ikitajwa kukua kwa wastani wa asilimia 7.2 na kuna uwezekano kiwango hicho kuongezeka katika siku za usoni.

Kulingana na Naibu Waziri wa Mali ya asili na Utalii Bwana Lazaro Nyalandu,katika kipindi cha miaka 15 Tanzania pekee imefaulu kuwavutia ziadi ya watalii 800,000 ambao wamechangia katika pato la taifa kiasi cha dola ya marekani bilioni 1.

Kwa hivi sasa serikali imeanzisha shabaha mpya kuboresha miundo mbinu ili kuwavutia watalii wengi zaidi.

Kongamano hili linafanyika barani afrika kwa mara ya kwanza na mara hii limewavutia mawaziri kutoka sehemu mbalimbali barani Africa.

Mwishoni mwa kongamano hilo wajumbewatapata fursa kuzunguka katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya kujionea shughuli za utalii.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031