Kituo kipya kuzinduliwa kusaidia wahamiaji wanaokwenda Afrika Kusini: IOM

Kusikiliza /

karibu Zimbabwe

Shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM na serikali ya Zimbabwe wanazindua kituo kilichokarabatiwa cha kupokea wahamiaji wanaovuka mpaka wa Msumbiji kuingia nchini humo wakielekea Afrika Ksini kwa ajili ya kutafuta kazi na hifadhi ya kisiasa.

Kituo hicho Nyamapanda kilichopo kilometa 300 Mashariki mwa mji mkuu wa Zimbabwe, Harare kitawezesha wahamiaji kupata huduma kama vile za kiafya, kisaikolojia, kijamii, chakula, makazi ya muda na zile za uhamiaji kwa watu takribani Mia Tatu wanaoingia Zimbabwe kuelekea Afika Kusini.

Wahamiaji watakaokidhi vigezo vya kupata hifadhi ya kisiasa watasafirishwa kwenda kambi ya Tongogara iliyoko kilometa 630 kutoka kituo hicho. Jumbe Omar Jumbe ni msemaji wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMAR JUMBE)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031