Kifo cha mfalme wa zamani wa Cambodia: Ban atuma rambirambi

Kusikiliza /

 

Mfalme Sihanouk enzi za uhai wake

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon ametuma salamu za rambi rambi kwa serikali na wananchi wa Cambodia kufuatia kifo cha mfalme wa zamani wa nchi hiyo Norodom Sihanouk aliyefariki dunia nchini China akiwa na wa miaka 89 kutokana na mshtuko wa moyo.

Taarifa ya msemaji mkuu wa Ban imesema Katibu Mkuu huyo ametambua jinsi Mfalme Sinahouk alivyojitoa kwa hali na mali wakati wa uhai wake kama kiongozi aliyeunganisha wananchi wa Cambodia na kutambuliwa na kuheshimiwa ndani na nje ya nchi yake.

Ban amesema ni matumaini yake kuwa mchango wa mfalme huyo wa zamani waCambodia  kuendeleza mchakato wa maridhiano nchini humo unaojumisha haki utaendelezwa.

Mfalme Sihanouk alikuwa akiishi China kwa kipindi cha miaka minane iliyopita ambapo alishika kiti cha ufalme kwa miaka 60 tangu mwaka 1941 hadi alipokasimu kiti hicho kwa mwanae Norodom Sihamoni mwaka 2004.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031