Kesi dhidi ya Charles Taylor kukamilika karibuni: Jaji Avis-Fisher

Kusikiliza /

Shireen Avis Fisher Mahakama maalum ya Sierra Leone inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa imesema iko katika hatua za mwisho za kumaliza kesi yake ya mwisho ambayo ni ile inayomhusu Rais wa zamani wa Liberia, Charles Taylor.

Rais wa mahakama hiyo Jaji Shireen Avis Fisher ametoa taarifa hizo leo mbele ya kikao cha Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani wakati huu ambapo mahakama hiyo inatarajiwa kumaliza muda wake mwezi Septemba mwakani..

“Hukumu ya mwisho itaamua iwapo Taylor ana hatia au la ambapo mahakama hiyo itaingia katika kipindi cha kufunga pazia ya kazi zake na kumaliza kabisa. Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai kufanya hivyo."

Mahakama hiyo maalum kwa Sierra Leone ilianzishwa muongo mmoja uliopita kwa ajili ya kuwafungulia mashtaka wakiukwaji wa sheria za kibinadamu za kimataifa na kitaifa wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031