Katibu Mkuu wa UM apongeza mabunge ya Sudan na Sudan Kusini

Kusikiliza /

rais Omar Al-Bashir wa Sudan na Salva Kiir wa Sudan Kusini

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amepongeza mabunge ya Sudan na Sudan Kusini kwa kuridhia mikataba ya ushirikiano kati ya nchi mbili hizo iliyotiwa saini mwezi uliopita na marais wao Salva Kiir wa Sudan Kusini na Omar Al Bashir wa Sudan..

Ban amekaririwa na msemaji wake akizitaka nchi mbili hizo sasa kutekeleza makubaliano hayo mara moja ikiwemo kuanza kazi kwa mfumo wa pamoja wa kufuatilia na kuweka mipaka yao sawa.

Sudan Kusini ilipata uhuru wake kutoka Sudan mwaka jana hata hivyo kumekuwepo na mizozo baina yao kuhusiana na masuala kadhaa ikiwemo mipaka. George Njogopa na taarifa zaidi.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031