Katibu Mkuu wa UM alaani mauaji ya askari wa UNAMID

Kusikiliza /

KM Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amelaani vikali shambulio la kushtukiza huko Darfur, Sudan, dhidi ya msafara wa askari na watumishi wa kiraia walio katika kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika, UNAMID, lililosababisha kifo cha mlinda amani mmoja kutoka Afrika Kusini na kujeruhi wengine wa tatu.

Msemaji wa Ban, amemkariri Katibu Mkuu huyo akitoa pole kwa serikali ya Afrika Kusini, UNAMID na familia za askari huyo huku akitaka uchunguzi ufanyike juu ya tukio hilo na wahusika wafikishwe mbele ya sheria.

Kwa mujibu wa UNAMID, shambulio hilo la kushtukikza ni baya zaidi dhidi ya kikosi hicho kwenye eneo hilo ndani ya wiki mbili na limetokea baada ya watu wasiofahamika kushambulia ghafla msafara huo uliokuwa ukitokea Kutum kuelekea mji wa Hashaba kutathmini hali ilivyo baada ya ripoti za kuwepo kwa ghasia eneo hilo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031