Jumuiya ya Ulaya yatakiwa kuwapa hifadhi na usalama watafuta hifadhi kutoka Syria

Kusikiliza /

wakimbizi wa Syria

Zaidi ya Wasyria 16,000 wametuma maombi ya kutaka kupewa hifadhi kwenye Jumuiya ya Ulaya kwa muda wa miezi 18 iliyopita kwa mujibu wa shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR. Kati ya mataifa yaliyopokea kiwango kikubwa cha maombi ni pamoja na Ujerumani, Sweden na Uswisi.

UNHCR inatoa wito kwa wanachama wa Jumuiya ya Ulaya kuipa nafasi kubwa nchi ya Syria wanaposhughulikia maombi hayo na kutowarudisha kwa lazima wanaotafuta hifadhi. Adrian Edwards kutoka UNHCR anasema kuwa wanachama wa Jumuia ya Ulaya wanaweza kuwapa watafuta hifadhi kutoka Syria makao ya muda kukiwa na matumani kuwa mzozo ulio nchini humo utaisha na watu hao kurudi makwao.

(SAUTI YA ADRIAN EDWARDS)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031