Jopo la wataalam wa UM lataka ulinzi kwa wanafunzi na wanaharakati Pakistani

Kusikiliza /

Margaret Sekaggya

Jopo la wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa wanaotetea haki za binadamu, uhuru wa kujieleza, elimu na kupinga mauaji , wameitaka serikali ya Pakistani kuhakikisha wanafunzi hususan wa kike wanalindwa na kwamba makundi yenye msimamo mkali hayazuii uwezo wa raia wa kawaida kutekeleza haki zao za kibinadamu.

Wametoa kauli hiyo mjini Geneva, Uswisi kufuatia kitendo cha kikundi kimoja cha kitalibani nchini Pakistani, cha kujaribu kumuua Malala Yousafzai, mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 14 aliyejitokeza hadharani kutetea elimu ya mtoto wa kike.

Margaret Sekaggya ambaye ni mtaalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu watetezi wa haki za binadamu amesema serikali ya Pakistani inapaswa kufanya kila jitihada kumlinda binti huyo na wengine wote wanaofanya kazi kutetea haki za mwanamke na mtoto wa kike.

Naye mtaalam anayepinga mauaji ya kinyume cha sheria, Christof Heyns, ametaka uchunguzi wa kina na wa haraka dhidi ya shambulio hilo na kwamba apatiwe ulinzi yeye na wengine wanaowindwa na vikundi vyenye msimamo mkali.

Kwa upande wake Kishore Singh ambaye ni mtaalam kuhusu haki ya elimu ametaka serikali ya Pakistan kushutumu wazi kitendo hicho na kuunga mkono bayana haki ya watoto wote hususan wa kike nchini humo kwenda shule bila woga wala kushambuliwa.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031