Jitihada zaidi zahitajika katika kulinda maeneo ya hifadhi ya bayo-anuai: UNEP

Kusikiliza /

eneo la hifadhi la bayo-anuai

Ingawa idadi ya maeneo ya hifadhi, na mbuga za wanyama imeongezeka kote duniani, nusu ya maeneo yenye bayo-anuai ya kuaziziwa zaidi hayana ulinzi wowote. Haya ni kwa mujibu wa ripoti ya uchunguzi mpya wa Shirika la Mpango wa Mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP, ambao unafuatilia maendeleo yanayofanywa kuhusu malengo ya kimataifa yaliyoazimiwa kuhusu maeneo ya hifadhi ya ulimwengu.

Ripoti hiyo ambayo imewasilishwa kwenye kongamano la kumi na moja la Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Bayo-anuai, inaonyesha kuwa maeneo yenye kulindwa yanadhibitiwa kwa njia ya usawa, huku jamii za asili zikipewa nafasi muhimu katika kuyalinda na kunufaika nayo.

Licha ya hayo, ripoti inaonyesha kuwa uwekezaji wa hivi sasa katika maeneo ya kulindwa ni nusu tu ya kile kinachohitajika kusaidia viumbe vilivyo katika hatari ya kuangamizwa, kulinda mazingira yanayohatarishwa na kupata matunda kamili ya udhibiti endelevu wa maeneo ya hifadhi.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2017
T N T K J M P
« jun    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930
31