ITU na WHO zakubaliana kuhusu mpango wa kupunguza gharama na kuokoa maisha

Kusikiliza /

simu za mkononi

Mkakati mpya wa kutumia teknolojia ya simu za mkononi kusaidia kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza, umezinduliwa na Shirika la Kimataifa la Mawasiliano, ITU kwa ushirikiano na Shirika la Afya Duniani, WHO, mjini Dubai. Teknolojia hiyo, hususani ujumbe mfupi na apps, inatarajiwa kutumiwa katika kukabiliana na magonjwa kama kisukari, saratani, maradhi ya moyo na mengineyo yanayoathiri viungo vya kupumua.

Magonjwa haya yasiyo ya kuambukiza ni miongoni mwa sababu kuu ya vifo katika nchi zilizoendelea kama ilivyo katika zile zinazoendelea. Magonjwa haya pia huongoza katika mahitaji na gharama ya afya katika nchi zilizoendelea na zile ambazo zina vipato vya wastani.

Kati ya vifo milioni 57 kote duniani, magonjwa yasiyo ya kuambukiza yanakadiriwa kusababisha hadi vifo milioni 36 kila mwaka, wakiwemo watu milioni 14 wenye umri wa kati ya miaka 30 na 70. Kwa kutumia teknolojia ya simu za mkononi, inatazamiwa kuwa uhai utaokolewa, magonjwa na ulemavu utapungua na gharama za huduma za afya zitapungua kwa kiasi kikubwa. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031