IOM yauganisha watoto 51 na familia zao nchini Uganda
Kusikiliza /Shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa, IOM limewarejesha katika familia zao watoto 51 nchiniUgandaambao walisafirishwa kutoka vijijini hadi mijini hususan mji mkuuKampala.
IOM imesema watoto hao waliorejeshwa huko Karamoja, kaskazini mwaUganda, waliletwa mjini na kujikuta wakilazimika kuwa ombaomba mitaani au wezi na hata kutumikishwa majumbani au kuokota vyuma chakavu. Hali hiyo ilifanya watoto hao waliokoseshwa elimu kukumbwa na matatizo ikiwemo vipigo na ubakaji.
Mkuu wa IOM nchini Uganda, Gerard Waite amesema mpango wa kuunganisha watoto hao na familia zao ni mgumu na unahitaji uratibu wa hali ya juu na mashirika yasiyo ya kiserikali, vyombo vya habari, na serikali ili kulinda watoto hao.
Hata hivyo amesema ili kuzuia tatizohiloni lazima kubaini sababu ya watoto kusafirishwa kinyume cha sheria hadi mijini.
