IOM kuzinda mradi wa kusaidia jamii tofauti kuishi kwa amani Afrika Kusini

Kusikiliza /

Afrika Kusini

Shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM mwezi huu litazindua mradi wa miezi mitatu wenye lengo la kujenga na kuimarisha amani kwenye jumuiya za watu wanaotoka jamii tofauti nchini Afrika Kusini.

IOM imepata msaada kutoka benki ya maendeleo kusini mwa Afrika, DBSA na shirika la maendeleo ya viwanda IDC na mradi utatekelezwa kwenye jimbo la Western Cape nchini Afrika Kusini kupitia shirika lisilo la kiserikali, ARESTA lenye uzoefu wa kusimamia miradi ya kujenga utengamano kati ya wahamiaji na wenyeji na utawezesha jamii husika kutatua migogoro yao pindi inapoibuka.

Mradi huu mpya unafuatia mafanikio ya mradi kama huo uliofanywa mwaka jana kwa lengo la kuongeza utangamano miongoni mwa jamii kwenye maeneo yaliyokumbwa na migogoro na kusababisha hata baadhi ya jamii kuona zimepuuzwa. George Njogopa na taarifa zaidi.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031