IOM kuwafunza watendaji wa Ethiopia

Kusikiliza /

wahamiaji wa Ethiopia

Maafisa wa shirika la Umoja wa Mataifa wanaohusika na uhamiaji IOM wataendesha mafunzo ya siku tatu kwa watendaji wanaoratibu ofisi zinazojihusisha na raia wa Ethiopia waliko nchi za ng'ambo.

Mafunzo hayo yanayotazamiwa kuanza Oktoba 15 yanatazamiwa kuendeshwa mjini Addis Ababa yatakuwa na lengo la kuwajengea uwezo watendaji hao.Washiriki wa mafunzo hayo ni kutoka majimbo ya Amhara, Tigray, Dire Dawa na Gambella.

Mada kubwa zitakazo zingatiwa ni pamoja na uhamiaji,maendeleo na sera za nchi kuhusiana na raia walioko nchi za ng'ambo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031