India inatakiwa itekeleze sheria za kulinda haki za wanawake: UM

Kusikiliza /

 

Michelle Bachelet

Mkurugenzi Mkuu wa kitengo cha wanawake kwenye Umoja wa Mataifa, UN Women, Michelle Bachelet, amesema kuwa taifa la India linafaa kutekeleza sheria ilizo nazo ili kulinda haki za wanawake. Bi Bachelet amesema hayo mbele ya ziara yake nchini India, ambayo amesema itaangazia kuchagiza juhudi za kuendeleza usawa wa kijinsia na kuwapa wanawake uwezo kwenye ngazi zote, zikiwemo vijijini.

Bi Bachelet ameipongeza India kwa hatua zilizopigwa katika kuweka sheira na mikakati ya kuendeleza haki za wanawake, zikiwemo mswada unaohusu ukatili wa ngono, sheria dhidi ya dhuluma za nyumbani, na ile inayohusu ajira kwa watu vijijini yenye lengo la kuhakikisha usawa wa ujira kwa wanawake.

Licha ya hatua hizo, Bi Bachelet amesema ataitumia ziara yake nchini humo kutoa wito kwa serikali ya India kuchukua hatua mathubuti kwa haraka ili sheria hizo nzuri zitekelezwe kwa manufaa ya wanawake wa matabaka yote. Ameongeza kuwa, kwa sababu ya idadi yake ya watu bilioni 1.22, India inaweza kuongoza kote ulimwenguni katika nyanja mbalimbali. George Njogopa na taaifa kamili

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031