IMF yawataka serikali zikabiliane na matishio yanayokabili kuimarika uchumi

Kusikiliza /

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa, IMF, Christina Lagarde, ametoa wito kwa viongozi duniani kukabiliana mara moja na hali ya hatari inayoendelea kuukabili uchumi wa kimataifa. Bi Lagarde amesema hatua za ushirikiano zinatakiwa kuchukuliwa na nchi zote wanachama wa IMF, wakati taasisi hiyo ikifungua mikutano yake ya kila mwaka. Mikutano ya Benki ya Dunia na IMF inafanyika mjini Tokyo, Japan wiki hii.

Mapema wiki hii, IMF katika ripoti yake ya hali ya fedha ya kimataifa ilotolewa mjini Tokyo, ilisema kuwa kuimarila kwa sekta ya kimataifa ya fedha kunaendelea kuhatarishwa kwa kiasi kikubwa, huku masoko ya fedha yakiyumbayumba na wanasera wa Ulaya kuhangaika na matatizo yaliyopo sasa.

Lagarde amesema kupotezwa kwa imani katika masoko kumewafanya wawekezaji kutoka nchi zilizo nje ya eneo la Euro kuanza kupeleka fedha zao kwenye eneo la Euro, na hivyo kuongeza gharama ya mikopo katika nchi hizo.

Mkuu huyo wa IMF amesema viongozi wa kifedha watajaribu kuchagiza ukuaji wa uchumi wa kimataifa, akisema kuwa watafanya kile kinachotakiwa kufanyika, na kuhakikisha kuwa uchumi wa kimataifa haukwamuliwi kwa kiwango kidogo tu, bali ni utakuwa tena kwa muda mrefu.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031