Idadi ya watumiaji wa simu za mkononi imefikia bilioni 6: ITU

Kusikiliza /

simu ya mkononi

Idadi ya watu wanaotumia simu za mkononi kote duniani imefikia bilioni sita, kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Mawasiliano, ITU. Idadi hii, inamaanisha kuwa, kwa kila watu mia moja kote ulimwenguni, watu themanini na sita wana simu za mkononi.

Shirika hilo la ITU linasema, zaidi ya watu bilioni 2.3, ambao ni zaidi ya thuluthi moja ya idadi ya watu hao kote duniani, wameunganishwa kwenye mtandao wa Internet. Katika ripoti yake ya kila mwaka ya kupima mawasiliano katika jamii, ambayo inafuatilia maendeleo katika sekta ya teknolojia ya haabari na mawasiliano, ITU inasema ukuaji huu wa kasi umetokana na kuongezeka ushindani baina ya watoaji wa huduma za mawasiliano, ambao umechangia gharama ndogo kwa watumiaji wa simu za mkononi.

Ripoti hiyo inasema Jamhuri ya Korea Kusini ndiyo nchi iliyoendelea zaidi katika sekta ya teknolojia ya habari na mawasiliano, ikifuatiwa na Sweden, Denmark, Iceland na Finland. Susan Teltscher ni msimamizi wa kitengo cha takwimu za teknolojia ya habari na mawasiliano katika ITU.

Viwango vya ukuaji wa matumizi ya simu za mkononi vimekuwa asilimia 40 kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita, na hii imechangia sana kubadili hali kwa sababu ukuaji mwingi zaidi unaonekana katika nchi zinazoendelea, ambako huduma hizi hazikuwa hadi hivi majuzi tu. Kwa mara ya kwanza katika ripoti yetu tumeangalia kipindi cha miaka minne, tangu mwaka 2008 hadi 2011, ambako tumefuatilia gharama ya huduma za habari na mawasiliano, na kutambua kuwa gharama ya huduma hizo ilishuka kwa asilimia 30 katika kipindi hicho. Kupungua huko kulikua mkubwa zaidi katika nchi zinazoendelea. Kwa hiyo, kuongezeka kwa huduma na gharama kuwa nafuu, vyote kwa pamoja vimechangia ukuaji huu.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031