Hungary iwajibishe viwanda vinavyochafua mazingira: UM

Kusikiliza /

Calin Georgescu

Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa, Calin Georgescu amesifu hatua ya serikali ya Hungary ya kushughulikia madhara ya mtambo wa kiwanda cha chuma cha Ajka mwaka 2010 huku akitaka hatua zaidi zichukuliwe ikiwemo kurekebisha sera za uchafuzi wa mazingira ili kampuni zinazohusika na uchafuzi wa aina hiyo ziwajibishwe zaidi.

Georgescu amesema hayo wakati wa ziara yake ya siku nane ya tume huru anayoongoza iliyotumwa na Kamisheni ya haki za binadamu ya umoja wa Mataifa kuchunguza madhara ya kisa hicho kilichokumba wakazi wa maeneo ya Kolontar na Devecser.

Amesema haki inakuwa imepotea pindi wananchi wanapojikuta wakilipia uzembe wa wale waliosababisha madhara hayo na kusema kuwa bado ana wasiwasi juu ya hali hiyo iwapo suala la kuwajibisha viwanda vikubwa vinavyochafua mazingira nchini Hungary halipatiwa uzito.

Uchafuzi wa mazingira huko Ajka ulisababisha vifo na majeruhi kwa wakazi jirani na kiwanda hicho pamoja na uharibifu wa mazingira uliogharimu karibu dola Milioni 910 hadi sasa kurejesha hali ya kawaida. Ripoti kamili ya ziara ya Georgescu ikijumuisha mapendekezo ataiwasilisha mwezi Septemba mwakani katika kikao cha Kamisheni ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031