Hatua zimepigwa katika kuhifadhi jenetikia tofauti za mifugo: FAO

Kusikiliza /

wanyama

Huku nchi nyingi zikiwa zinachukuwa hatua kusitisha uharibifu wa rasilmali za jenetikia ya mifugo, ambazo ni muhimu kwa chakula na kilimo, bado kuna mwanya mkubwa ambao unatakiwa kukabiliwa kwa haraka. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti za Shirika la Chakula na Kilimo, FAO, ambazo zimewasilishwa leo katika kongamano la kimataifa kufuatia utafiti uliofanywa katika nchi 80.

Utafiti huo ulihusu hatua zilizopigwa katika kutekeleza mpango wa hatua za kimataifa kuhusu jenetikia ya mifugo.

Ripoti hizo zinaonyesha kuwa serikali zinaanza kuweka mikakati ya kukabiliana na kupungua kwa aina za kiasili za mifugo. Kwa mujibu wa ripoti hizo, hatua kubwa zimepigwa katika nchi zinazoendelea, lakini nchi nyingi barani Afrika, Amerika ya Kusini na Karibi zimebaki nyuma katika kutekeleza hayo. Alice Kariuki na taarifa kamili.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031