Hatua zaidi zahitajika kudhibiti utumwa Kazakhstan

Kusikiliza /

Gulnara Shahinian

Kazakhstan iko hatarini kupoteza mafanikio yake iliyopata ya kudhibiti utumwa nchini humo iwapo sheria na mbinu mpya zinazotungwa kudhibiti vitendo hivyo hazitashirikisha sekta zote zinazoguswa na vitendo hivyo kama vile serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali, ya kimataifa na sekta binafsi.

Mtaalamu wa umoja wa Mataifa kuhusu utumwa wa nyakati za sasa Gulnara Shahinian ametoa tahadhari hiyo mwishoni mwa ziara yake ya siku nane nchini Kazakhstan ambapo alipata fursa ya kuzungumza na maafisa mbali mbali waliomweleza vikwazo wanavyopata ikiwemo sheria za ajira zinazotaka wahamiaji kutoa taarifa zaidi kabla ya kupatiwa kibali cha kazi.

Walimu nao walieleza kwamba watoto wa wahamiaji haramu wanazuiwa kusoma licha ya kwamba wao wako tayari kuwafundisha bila malipo ali mradi wawaepushe na mazingira hatarishi ya kazi wakati huu ambapo familia za watoto hao haziwezi kupata huduma ya afya isipokuwa wakati wa dharura.

Mtaalamu huyo pamoja na kuishukuru Kazakhstan kwa kushughulikia suala hilo, amesema kuondoa utumwa kunahitaji suluhisho la kudumu ikiwemo kuweka mfumo rahisi wa kupata vibali vya ajira na kuhakikisha raia na wahamiaji wanapata huduma za afya na elimu ili kulinda mafanikio yaliyokwishapatikana ya kupambana na utumwa.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031