Harakati za kutokomeza umaskini zinatishiwa na uhaba wa fedha: Ban

Kusikiliza /

kuadhimisha siku ya kutokomeza umaskini

Wakati dunia leo inaadhimisha siku ya kutokomeza umaskini, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema jitihada za kutokomeza umaskini zinakumbwa na tishio la uhaba wa fedha katika kipindi hiki ambacho serikali zinachukua hatua kali za kubana matumizi ili kuinua uchumi.

Ban amesema licha ya hatua hizo, huu ni wakati wa kuhakikisha maskini wanapata huduma kama vile za kijamii, kipato cha uhakika, hifadhi ya kijamii na ajira yenye staha.

Ametoa mfano kuwa kwa sasa kiwango cha mafukara kimepunguzwa kwa asilimia 50 lakini bado zaidi ya watu Bilioni Moja wanaishi maisha ya kimaskini wakinyimwa haki yao ya chakula, elimu na afya.

Katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amesema ni kwa kufanya hivyo tu ndipo inawezekana kujenga jamii thabiti na yenye matumaini na siyo kuhangaika kuwa na bajeti zinazokandamiza maskini.

Amesema jitihada zote zinapaswa kufanyika ili kuhakikisha nchi zote zinafikia malengo ya milenia mwaka 2015.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031