Guatemala kuongoza Baraza la Usalama mwezi huu wa Oktoba

Kusikiliza /

Balozi wa Guatemala, Gert Rosenthal, Rais wa Baraza la Usalama

Guatemala, nchi ya Amerika ya Kati kwa mara ya kwanza imechukua uenyekiti wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa mwezi huu wa Oktoba ambapo imeeleza bayana kuwa masuala ya amani na haki yatakuwa ajenda ya juu wakati wa kipindi hicho.

Balozi wa Guatemala katika Umoja wa Mataifa Gert Rosenthal amesema suala muhimu ni uhusiano kati ya Baraza hilo la usalama na mahakama ya kimataifa ya makosa ya uhalifu, ICC.

Tumechagua kwa mara ya kwanza kuwa na mjadala juu ya kile tunachoita amani na haki suala ambalo kiukweli linaangalia mtangamano kati ya baraza la usalama la umoja wa mataifa ambalo ni chombo cha kisiasa na ICC ambacho ni chombo cha kisheria na vile ambavyo shughuli zao zinaingiliana. Pia tutaangalia jinsi ambavyo majukumu ya ICC yenye jukumu la kudhibiti uonevu duniani inaweza kuwa chombo muhimu katika kusaidia matumizi ya diplomasia ili kuepusha matatizo.

Guatemala ni miongoni mwa mataifa matano ambayo kwa mwaka huu na mwakani yatakuwa na ujumbe usio wa kudumu katika katika Baraza la Usalama ambalo jukumu lake ni kusimamia amani na ulinzi duniani kwa kupitisha maazimio yanayohusi nchi zote wanachama.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031