FAO na Jumuiya ya Ulaya waungana kupiga vita njaa

Kusikiliza /

Rais wa Tume ya Ulaya José Manuel Barroso amekutana na Mkurugenzi mkuu wa shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO José Graziano da Silva mjini Brussels ambapo wawili hao walikubaliana kuwa Jumuiya ya Ulaya ndiyo mshirika mkuu wa FAO na hivyo ni lazima itekeleze wajibu wake kikamilifu. Wawili hao pia walizungumzia suala la usalama wa chakula yakiwemo maendeleo na sera kuhusu lishe.

Kwa sasa kuna karibu watu milioni 870 ambao hawana chakula cha kuwatosha kote duniani wakati zaidi ya watoto milioni 2.5 wakiaga dunia kila mwaka kutokana na utapiamlo. Bwana Barrosso amesema kuwa wao na FAO ni washirika wakuu katika vita dhidi ya utapiamlo kwenye nchi maskini na katika kuchangia kuwepo kwa usalama wa chakula duniani

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031